Thursday, May 11, 2006

ukimya kwenye maswala ya ngono na madhara yake
hapa kwetu Tz kama mahala pengi afrika na kwingineko si jambo la kawaida kukuta watu wanazungumzia mambo ya ngono hadharani na hata kwenye vyou vyetu vikuu hili swala ni nadra sana kulikuta kwenye masomo yetu tunayochukua.Hii ni pamoja ya kwamba karibu kila binadamu alityemzima anashiriki tendo hili.
swali langu ni je?kwanini kitendo hichi ambacho ni cha kawaida kabisa tena cha asili hakizungumzwi kabisa??Hii ina ishara gani??tunazungumzia vitu vingi sana vifo,vyakula,uchumi,mazingira?nk kwanini ngono halizungumzwi kwenye vikao vyetu vya umbea??kwanini ni la siri kiasi hiki??
kuna mtu aliniuliza swali kwamba hivi ukiona watu hawapendi kulizungumza jambo fulani unapata tafsiri gani?? nikasema ni vigumu labda hawataki lijulikane ila nikafikiri tena kwamba binadamu siku zote hataki mambo yake mabaya au ya aibu yajuklikane kwa watu wengi,basi nikajibu kuwa jambo ambalo watu hawalizungumzi ni jambo baya.Sasa hivi ngono ni mbaya ndo maana watu hawalizungumzi??
kutokuzungumzia maswala ya ngono hadharani sasa kunatuumbua kwa sababu watu wanapuputika na jamii haijui ifanyeje kwasabau ugonjwa huu unaambukizwa kwa ngono,jambo lile lile ambalo kila mtu hayuko tayari kulizungumzia kwa hiyo unakuta wazazi hawawezi kuzungumza na watoto wao juu ya swala hili,waalimu pia wanapata shida kulifundisha vizuri mashuleni.Watoto kwa sababu wameaambiwa kuwa huo ni mchezo mbaya kwa hivyo hawawezi kulizungumzia kati yao wenyewe kwa sababu utaonekana we ni muhuni na una tabai mbaya.Sasa virusi vinatumia mwanya huo kusambaa.kwa sababu hakuna aliye tayari kusema hadharani kuwa yeye ameshiriki ngono isiyo salama.na hakuna anayekubali kuwa yeye anshiriki ngono na watu wengi.
nyakati hizi zinahitaji watu tuzungumzie mambo ya ngono na watoto wetu,wadogo zetu,wanafunzi wetu,marafiki zetu ili tupeane taarifa sahihi na muhimu kwa maisha yetu.Ngono si salama tena na si jambo la siri tena kwa sababu ukimwi umetuonyesha naman watu wasivyo waaminifu.Ni lazima sasa tuifanye mada ya ngono kuwa ya kawaida badala ya kuificha.Tusiwaache watoto wajue ngono siku ya kwanza wanapofanya tendo hilo,au wajue ngono kupitia mitandao inayopotosha au majarida yanayo fanya biashara tu yasiozingatia maadili na madhara yanoyoletwa na michapisho yao wala tusiruhusu wakajua kupitia mikanda au cd za ngono zilizotapakaa mitaani,kwa sababu wakijua kupitia huko basi taarifa hizo zitawapotosha na zitawafanya wahanagamie.
kutokuzungumzia ngono ndio inafanya wasichana wengi waishie vitandani na wanaume bila kinga,bila hiari au utayari na maandalizi ya kutosha,na wanaume kwasabu ni waroho wa jambo hilo wanajisahau kwamba wanahatarisha afya zao wenyewe huku wakijivunia kuwa wameweza kulala na msichana na hivyo kuuthibitsha urijali na uume wao.Enzi hizo mi nadhani zimepitwa na wakati.wale tulio kwenye mahusiano tuzungumze tuseme mapema kwamba leo bwana tukafanye ngono lakini je tuna vifaa??yaani kinga? kwa namna hii mi nafikiri vijana wengi wataweza kuwa na usemi zaidi juu ya mahusiano yao.Ila tukiendelea kunyamazia ngono tendo tamu kuliko zote lakini tendo ambalo sasa hivi ni hatari kuliko yote basi hata vita vyetu dhidi ya ukimwi.imaskini na maradhi yatagonga mwamba.

6 comments:

Jeff Msangi said...

Ukiliangalia suala hili kwa kuzingatia mila na desturi zetu utagundua kwamba ngono inaongeleka na imekuwa ikiongeleka tangu enzi na enzi.Tulikuwa na utaratibu maalumu,kulikuwa na jando,unyago nk.Ila kama unachotaka kukiona ni sisi nasi kuiga utamaduni wa kimagharibi wa kuongelea ngono kama vile chakula nadhani unakosea na pengine hapo ndipo tunapozidi kupotea kabisa waafrika.Tunachotakiwa ni kuboresha mila zetu na kuacha kuiga kila kitu kutoka magharibi

Christian Bwaya said...

Nakubaliana na mtazamo wako, bwana Albert, kwamba tunahitaji kuanza kuvunja upya kimya katika kuzungumzia mambo haya yanayohusiana na ngono. Kwamba jamii zetu, za kiafrika kwa mukhtadha huu, zielimishwe juu ya kutoa elimu ya mahusiano kwa watoto na vijana ili kuweza kuwawahi mapema kabla ya tatizo kuwa kubwa.

Tunajua kuwa utamaduni huu hauko miongoni mwetu. Wazazi hawasemi na watoto wao kuhusu mambo haya. Walimu ndio kabisaa usiseme. Lakini ajabu ni kwamba mambo haya watoto wanayatafiti kimya kimya, na bahati mbaya ni kwamba wanayajua kwa namna mbovu inayoathiri ufahamu wao katika mambo ya ngono.

Hapa ndiko tatizo la UKIMWI linakochipukia. Kwamba tuajikuta tukiwa na jamii yenye wapenda ngono zisiozingatia maadili yenyewe hasa. Kwamba watu wanajikuta wakidhani urafiki wowote na mwana dada ama kaka unamaanisha ngono! Mtazamo ambao hata tukisisitiza cofta (kondomu) bao linakuwa ni bila bila.

Ninadhani Msangi anaposema tuziboreshe mila zetu, ana maana ya kuziangalia upya. Zile zinazosaidia tuziendeleze. Zenye matatizo kama hizi za kila kitu kimya kimya, tuzipe mkono. Maboresho hayo ndiyo yanayoweza kutusaidia kupingana (kwa mafanikio) na janga la UKIMWI/VVU.

jakogallo said...

Bwana msangi, jando na unyago ni nzuri sana hasa enzi hizo.lakini kumbuka wakati huo ukimwi haukwepo,wakati huo watu walisubiri kuoana ndipo wafanye ngono,wakati huo chanzo cha maarifa au habari ilikuwa ni watu maalum katika jamii.mambo haya yote siku hizi yamebadilika.ngono kabla ya ndoa ni kawaida tena unategemewa kijana ukishabalehe tu watu wanafurahi kukuona unatania tania visichana nk,vyanzo vya habari ni vingi hakuna anayejitamba kuwa yeye habari fulani anaijua peke yake,na ukimwi upo.
kitu kingine.christian anasema kweli kuwa katika kuboresha huko basi yale ambayo hayawezi kutusaidia leo tuyaache.jando na unyago zote siku hizi zimeamia mashuleni na mashirika ya dini na yote hayo yamekaa katika mfumo wa kimagharibi zaidi.kwa ufupi hakuna wataalamu wala wateja wa jando na unyago sikuhizi.na hata jando na unyago unayosema ndio zimeleta ukandamizwaji kwa wanawake mpaka wasiwe na usemi juu ya maswala ya ngono.kwa sababu walifunzwa kuwa hawaruhusiwi kuwakatalia waume zao na wanaume walifunzwa kuwa na usemi juu ya ya mambo ya ngono kwamba yeye ndio anaamua ni lini na ni vipi na wakati gani ngono ifanywe hata kama mwenzie hayuko tayari.mambo kama haya ndo yameleta madhara makubwa hasa wakati huu wa UKIMWI

Jeff Msangi said...

Bado naamini jando na unyago ni vitu vinavyoweza kuboreshwa ili viendane na karne hii au wakati tulionao.Tatizo letu ni uvivu wa kufikiri na kudhani kwamba tunaendelea kwa kuacha mila na desturi zetu na kuutamani umagharibi zaidi.Ninachoongelea mimi ni kuboresha mila na desturi zetu na sio kuzirudia kama zilivyokuwa.Natambua mabadiliko ya dunia yetu.

Jaduong Metty said...

Waingereza wana neno "taboo" na ngono ni moja wapo. Kila kitu ambacho ni "taboo" watu tunakuwa na usongo nalo, lakini hakizungumzwi..ni kama neno "nigger" hapa Marekani. Neno hili "linazungumzwa", lakini likizungumzwa kweli, utasikia mtu kapelekwa mahakamani..

Zaidi ya yote, nadhani umeuliza swali "tamu"..

Parmen said...

I 'm so glad you could come across this site ,
and we hope to establish good relations with you.
greetings from me ( Apotikobatbius.com ).
obat bius
obat tidur
apotik obat tidur

obat kuat
obat perangsang wanita

jual obat bius
jual obat tidur
apotik obat bius