ukimya kwenye maswala ya ngono na madhara yake
hapa kwetu Tz kama mahala pengi afrika na kwingineko si jambo la kawaida kukuta watu wanazungumzia mambo ya ngono hadharani na hata kwenye vyou vyetu vikuu hili swala ni nadra sana kulikuta kwenye masomo yetu tunayochukua.Hii ni pamoja ya kwamba karibu kila binadamu alityemzima anashiriki tendo hili.
swali langu ni je?kwanini kitendo hichi ambacho ni cha kawaida kabisa tena cha asili hakizungumzwi kabisa??Hii ina ishara gani??tunazungumzia vitu vingi sana vifo,vyakula,uchumi,mazingira?nk kwanini ngono halizungumzwi kwenye vikao vyetu vya umbea??kwanini ni la siri kiasi hiki??
kuna mtu aliniuliza swali kwamba hivi ukiona watu hawapendi kulizungumza jambo fulani unapata tafsiri gani?? nikasema ni vigumu labda hawataki lijulikane ila nikafikiri tena kwamba binadamu siku zote hataki mambo yake mabaya au ya aibu yajuklikane kwa watu wengi,basi nikajibu kuwa jambo ambalo watu hawalizungumzi ni jambo baya.Sasa hivi ngono ni mbaya ndo maana watu hawalizungumzi??
kutokuzungumzia maswala ya ngono hadharani sasa kunatuumbua kwa sababu watu wanapuputika na jamii haijui ifanyeje kwasabau ugonjwa huu unaambukizwa kwa ngono,jambo lile lile ambalo kila mtu hayuko tayari kulizungumzia kwa hiyo unakuta wazazi hawawezi kuzungumza na watoto wao juu ya swala hili,waalimu pia wanapata shida kulifundisha vizuri mashuleni.Watoto kwa sababu wameaambiwa kuwa huo ni mchezo mbaya kwa hivyo hawawezi kulizungumzia kati yao wenyewe kwa sababu utaonekana we ni muhuni na una tabai mbaya.Sasa virusi vinatumia mwanya huo kusambaa.kwa sababu hakuna aliye tayari kusema hadharani kuwa yeye ameshiriki ngono isiyo salama.na hakuna anayekubali kuwa yeye anshiriki ngono na watu wengi.
nyakati hizi zinahitaji watu tuzungumzie mambo ya ngono na watoto wetu,wadogo zetu,wanafunzi wetu,marafiki zetu ili tupeane taarifa sahihi na muhimu kwa maisha yetu.Ngono si salama tena na si jambo la siri tena kwa sababu ukimwi umetuonyesha naman watu wasivyo waaminifu.Ni lazima sasa tuifanye mada ya ngono kuwa ya kawaida badala ya kuificha.Tusiwaache watoto wajue ngono siku ya kwanza wanapofanya tendo hilo,au wajue ngono kupitia mitandao inayopotosha au majarida yanayo fanya biashara tu yasiozingatia maadili na madhara yanoyoletwa na michapisho yao wala tusiruhusu wakajua kupitia mikanda au cd za ngono zilizotapakaa mitaani,kwa sababu wakijua kupitia huko basi taarifa hizo zitawapotosha na zitawafanya wahanagamie.
kutokuzungumzia ngono ndio inafanya wasichana wengi waishie vitandani na wanaume bila kinga,bila hiari au utayari na maandalizi ya kutosha,na wanaume kwasabu ni waroho wa jambo hilo wanajisahau kwamba wanahatarisha afya zao wenyewe huku wakijivunia kuwa wameweza kulala na msichana na hivyo kuuthibitsha urijali na uume wao.Enzi hizo mi nadhani zimepitwa na wakati.wale tulio kwenye mahusiano tuzungumze tuseme mapema kwamba leo bwana tukafanye ngono lakini je tuna vifaa??yaani kinga? kwa namna hii mi nafikiri vijana wengi wataweza kuwa na usemi zaidi juu ya mahusiano yao.Ila tukiendelea kunyamazia ngono tendo tamu kuliko zote lakini tendo ambalo sasa hivi ni hatari kuliko yote basi hata vita vyetu dhidi ya ukimwi.imaskini na maradhi yatagonga mwamba.
Thursday, May 11, 2006
Wednesday, May 10, 2006
Subscribe to:
Posts (Atom)